MAAJABU!! KIONGOZI WA MAKIRIKIRI AOKOKA
Kiongozi
wa kundi maarufu la Nyimbo za Asili la Makhirikhiri la nchini Botswana,
Mosesi Malapela a.k.a Shumba Ratshega, ametangaza kumrudia Mungu baada
ya kuokoka na kuanza kuhubiri neno la wokovu.
Habari za uhakika kutoka kwa Msemaji wa Kundi la Makhirikhiri Tanzania, Livingstone Mkoi zilieleza kuwa, kwa sasa kiongozi huyo amezaliwa upya baada ya kuachana na kila kitu cha kidunia na kuamua kumtumikia Mungu katika maisha yake.
Livingstone alifunguka: “Ni kweli Shumba amenieleza kuwa niwaambie Watanzania kuwa anawaheshimu na kuwakumbuka kutokana na mapokezi makubwa waliyompa mwaka 2010 alipofika Tanzania kufanya matamasha yake yaliyoandaliwa na Kituo cha Radio Times FM na kumpa mafanikio makubwa.
“Shumba anasema kuwa katika maisha yake mapya ya utumishi wa Mungu amekuwa akiiombea sana Tanzania pamoja na Rais Dk. John Pombe Magufuli.
“Kuhusu kuimba anasema ataendelea kuimba tu na kundi lake halitakufa kwa vile ule ni utamaduni wao wa asili.”
Mkoi aliongeza: “Tayari mtumishi huyo ameanza ujenzi wa kanisa lake kubwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo (Gaborone) kwa ajili ya kuhubiri Neno la Mungu.

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi