MAKONDA ASEMA SIOGOPI MASHMBULIZI

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda ametangaza mkakati mpya wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya, uhalifu pamoja watumishi wa halmashauri za manispaa wasiowajibika kwa wananchi katika jiji la DSM.

Akizungumza katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo na Rais John Pombe Magufuli, Bw. Makonda amesema Mwaka wa pili wa utumishi wake utaongeza makali ya mapambano hayo huku pia akitangaza kutorudi nyuma kutokana na baadhi ya watu kumshambulia.

Katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wabunge, wakuu wa wilaya , viongozi wa dini pamoja waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya, Mkuu wa mkoa amesema anafarijika kuona baadhi ya watumishi wanawatumikia wananchi ipasanyo, na kulisifu Jeshi la Polisi kwamba hivi sasa limebadilika na kufanya kazi kwa weledi na kutawaka viongozi wa dini kumuombea Rais John Magufuli na wasaidizi wake katika mapambano dhidi ya wabadhirifu wa mali za umma na wale wasiozingatia maadili ya Utumishi.


Baadhi ya Viongozi waliopata fursa ya kuongea katika hafla hiyo wamepongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa na kumuahidi ushirikiano.