DIAMOND PLUTNUM AVUNJA UKIMYA, AFUNGUKA KUHUSU UTAJIRI WAKE ANAVYOUPATA, WENGI WAPIGWA BUTWAA

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’, amefichua moja ya siri ya mafanikio yake makubwa kiuchumi ni kusaidia watu wenye uhitaji.
Diamond ambaye anatajwa kama msanii anayeongoza kwa kipato nchini, amesema anajisikia ufahari mkubwa kuona anaweza kuwasaidia watu wenye uhitaji na amekuwa akipata baraka zaidi kupitia kazi zake.

“Unajua watu wengi hawajui ukitoa unazidi kubarikiwa, hii kwangu imekuwa sehemu ya mafanikio sana, huwa najisikia mwenye bahati kubwa nikimsaidia mtu mwenye uhitaji kwani naamini lazima nitafanikiwa,” alisema Diamond.

Alisema amekuwa akikutana na changamoto nyingi ikiwamo watu wengi kuhitaji msaada kutoka kwake, lakini amekuwa akiwalenga wale ambao yeye anaamini wanahitaji msaada zaidi kwake.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.