BOSI WA CLOUDS MEDIA RUGE ATHIBITISHA MAKONDA KUVAMIA OFISI ZA CLOUDS AKIWA NA MAASKARI


Leo Jumatatu Machi 20,2017 mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ametoa ufafanuzi kuhusu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds Media Group usiku akiwa na askari wenye silaha wakati wa kipindi cha Shirika la Wambea Duniani (SHILAWADU)
Ruge- Alhamis tulikuwa na mkutano na TCRA,Kamati ya maudhui.

-Baadaye akaja Makonda,kisha akapotea nilipotoka ofisini nilikutana na wahusika wa kipindi cha Shilawadu


-Wahusika wa Shilawadu wakaniuliza wamerekodi kipindi waliomhoji mwanamke lakini stori haijabalance
-Jioni saa 10 nikapigiwa simu na Gwajima akiulizia kuhusu kipindi.

-Ijumaa SAA Tano usiku nikapigiwa simu kuwa Makonda amefika ofisini na askari wamefika ofisini na askari wakiwa na bunduki.

-Paul Makonda ambaye ni rafiki yetu ametukosea,huwezi kuja ofisini kwetu usiku na tena na mabunduki,Makonda ana namba zangu kwanini asinipigie,Paul alikuwa rafiki yetu tangu akiwa mkuu wa wilaya na mimi siwezi kukataa urafiki.

-Walipofika ofisini waliondoka na FLASH yenye kipindi.

-Hakuna mtu aliyepigwa ofisini.

-Makonda alitaka stori iruke wakati haijabalance,mimi kama msimamizi mkuu wa vipindi nilikataa.

-Ninachotaka tuiheshimu taaluma ya habari

-Vijana wa Shilawadu wameomba likizo wapumzike hawako vizuri.

-Sikukamatwa na polisi,nilienda kutoa taarifa kuhusu kilichotokea.

-Sisi Clouds Media tumeumia sana kwa haya aliyofanya Makonda.

-We want Respect,we want Heshima tu.

-Ishu imetokea Ijumaa niliamini Makonda atakuja kuomba radhi Jumamosi.

-Makonda ametumia vibaya madaraka yake.

-Makonda ni rafiki yangu kabla hata hajawa mkuu wa wilaya,lakini urafiki wa Bunduki sitaki,kwanza namzidi hata umri.

-Mimi namlaumu kwa kitendo alichofanya,kwanza alikua rafiki,kwanza ni mkuu wa mkoa,urafiki wa mtutu hauhitajiki.

-Kikubwa hatutaki kutengeneza hali yoyote ya kuyumbisha serikali,hatutaki kugombana na serikali.