ALIYEJERUHI WANNE KWA KISU AUAWA KWA KUPIGWA RISASI SINGIDA

Mkazi mmoja wa ikungi  mkoani singida amepigwa risasi na kufariki papo hapo ,baada ya kuwajeruhi kwa kisu watu zaidi ya wanne akiwemo mke wake  na  kuhatarisha maisha ya askari polisi wanne  kwa kutaka kuwachoma kisu  wakati wakitaka kumkamata.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba,amemtaja aliye pigwa risasi na kufariki marehemu  Herman Joseph miaka thelasini na mbili mkazi wa Ikungi madukani, baada ya kubishana na mke wake  alitoa kisu na  kumchoma makalioni , na watu walipo fika kutoa msaada aliwachoma kisu watu wengine watatu. 

Kamanda Magiligimba amesema baada ya skari kufika  marehemu Herman alifanya jaribio mara mbili la kutaka kuwachoma kisu askari licha ya askari kupiga risasi hewani ,lakini  askari mmoja katika jitihada za kukwepa kisu alianguka na maremu kumlalia askari huyo kwa kutaka kumchoma kisu kifuani,ndipo alipo fyatua risasi kwa kuokoa maisha yake na wengine na kusababisha kifo.


Kutokana na tukio hilo la marehemu kuchoma watu  visu kamanda Mgiligimba  alipoulizwa na ITV alisema kuwa marehemu alikuwa na matatizo ya akili  ambayo  huwa yana tokea na muda mwingine ana kuwa katika hali ya kawaida,pia amesema jeshi lake bado lina endelea na uchunguzi zaidi kubaini ukweli wa tukio hilo.