ZITTO KABWE: NIMEPATA KITU JUU YA MAHAKAMA NA KESI YA MBOWE
Nimetambua ( taken note ) uamuzi wa mahakama kuzuia amri ya kukamatwa ya mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA.
Nimefurahi kuwa Mwanasheria wa Act Wazalendo ndg. Albert Msando ni mmoja wa jopo la wanasheria wanaomtetea Mwenyekiti wa CHADEMA ndg. Freeman Aikaeli Mbowe.
Mfumo wa Vyama vingi nchini upo hatarini, ni LAZIMA wana mageuzi wote kuweka tofauti pembeni na kupambana kulinda Demokrasia yetu.
Tukiendekeza tofauti zetu ambazo nyengine ni za kijinga jinga tu, tutakuja shtuka hata hicho kinachotupa tofauti ( vyama ) hakipo.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi