MAHAFALI YA 46 YA UKWATA SHULE YA SEKONDARI BULUBA YAFANYIKA SHINYANGA

Wanafunzi wa kidato cha sita WANAUKWATA shule ya sekondari Buluba wanaotarajia kufanya mtihani wa kuhitimu mwaka huu wamefanya mahafali yao leo hii katika ukumbi wa EBENEEZER KKKT SHINYANGA ambapo mgeni rasmi Mchungaji na msaidizi wa Dean wa USHARIKA WA EBENEEZER KANISA KUU SHINYANGA Maganga.

Msaidizi wa Dean, Mchungaji Jackson Maganga akitoa ujumbe kwa wageni waalikwa na wanafunzi wanaotarajia kuhitimu masomo yao hivi karibuni.

 Akizungumza katika mahafali hiyo, mgeni rasmi amewasihi wanafunzi kuzidi kumtegemea Mungu kwani yeye ndio mweza wa mambo yote na yupo kwa ajili yao wamwitao. Pia akawaasa kuilinda imani hata baada ya masomo yao kwani hivi sasa wanaenda mtaani ambako kuna kila aina ya uovu hivyo wakilegea kidogo wanaweza wakajikuta wamepotea na kukosa umaana wa kukaa shuleni kwa muda wote huu.

Mahafali hiyo ya 46 tangu shule hiyo ianzishwe, ilifana sana kwani Mungu mwenyewe alionekana katika sherehe hiyo.katika masomo yao.
 Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu wakifuatilia jambo
Wanafunzi wanaohitimu wakimsikiliza nmchungaji wakati akitoa neno
 MC maadam Hellen akiwa katika ubora wake
 Kulia ni Mchungaji Maganga ambaye ni mgeni rasmi, katikati ni mtunza hazina wa tawi la Buluba na Jisoli Jisoli na kushoto ni Mlezi wa Ukwata Buluba Maadam Onolina Kikoti wakiendelea kufuatilia kinachoendelea ndani ya ukumbi.
 Boss wa wapishi Elizabeth Mittula akiwa tayari kwa ajili ya kuwahudumia wageni wote kwa chakula
 Bossi wa wapishi akiwa na mpishi wake mkuu Magreth Evance
 Kulia ni Usuil Charles akiwa na Pendo Charles wakifurahia jambo
Timu nzima ya wapishi wakiwa na bossi wao

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.