JINSI YA KUMFANYA MWANAO APENDELEE KUSOMA TANGU AKIWA MTOTO MDOGO

Hakuna mtoto anayezaliwa akiwa na uelewa wa kila kitu. Inabidi kufundishwa na wazazi au jamii inayo mzunguka. Aidha kwa wazazi au jamii inayomzunguka kukusudia, au yeye mwenyewe kuona na kuamua kuiga.
Yapo mambo ya muhimu inabidi mzazi au walezi kukusudia kuwekeza kwa mtoto, ikiwemo kupenda kujisomea vitabu, ili mtoto kuongeza uelewa. Tumewaacha watoto wetu wakikuzwa na Runinga, {tv} na pindi wanapokuwa kidogo tu tunawahamishia kwenye Social Media, kwa kuwapa simu za mikononi, bila kujua ni nini wanasoma na matokea ya yale wanayosoma kwenye simu zao au wanapoangalia tv. Taratibu tunajikuta jamii nzima tunakuza watoto wetu kama wale wa Hollywood, yaani wanaofanana na kwenye tamthilia wanazoziangalia kila siku, tena wenye malezi ya kuigiza, sio ya kweli.
Ni vizuri kumsogeza mtoto kwenye vitabu, kwanza utajua anasoma kitabu cha namna gani, na anaingiza nini kwenye akili yake. Tukipuuza hili, muda mfupi ujao wazazi tutajikuta tanatengeneza kizazi cha ajabu sana. 

Baadhi ya njia za kumfanya mtoto kupenda kusoma vitabu:-

1. Msomee mtoto wako tangia yupo mtoto:-
Mbali na vitu unavyomnunulia mtoto mara anapozalia, kama nguo, toys, diapers, nunua pia vitabu vinavyoendana na umri wake. Kisha msomee wakati ukiwa unapata muda naye wa utulivu, sio wakati analia. Ni vizuri kipindi ametulia, mnacheza naye, msomee mtoto wako hadithi utakazoona ni nzuri kwake. Unaweza kuona unapoteza muda, lakini unajenga mazoea mazuri sana, kwanza kwa mtoto wako na kwako pia. 
Inakufanya kupata muda na mtoto wako
mbali na simu zinazotufanya kukosa muda nao kwa kuperuzi 
 
Facebook au Whatsapp wakati wote na kusahau kama kuna watoto. Kaa chini na mtoto wako, kisha msomee tangia ni katoto kachanga. {Infant.}



2. Tembeleeni Maktaba {Library}, pamoja :-

Mtoto akishafikia umri wa kuanzia miaka miwili, anakuwa na michezo mingi sana. Ni ngumu kukaa naye chini na kumsomea, labda anapokuwa anausingizi. Na huo ndio wakati mwafaka wa nyinyi kuanza kutembelea maktaba. Akili yake itakutana na vitabu tu, na aina ya michezo itakayompelekea kusoma vitabu. Tafuta 
naye kitabu kwa kuangalia picha nje ya vitabu. Atakachoonekana kukipenda au kuvutiwa nacho, ndicho ukichukue. Kaa naye na kumsomea kwa muda mfupi. waweza kukichukua kitabu hicho na kurudi nacho nyumbani, ili kuendelea kumsomea, mara kwa mara.



3.Jitahidi kumsomea mtoto wako mara kwa mara:-

Tafuta wakati muafaka kwako wewe kwanza, ambapo sio simu wala tv na wewe itakufanya uonekana hujatuliza mawazo yako kwa watoto. Zima simu, au Weka mbali vitu vyote vitakavyokufanya usitulize akili, ili na watoto nao waone mnafanya kitu kizuri. Kadhalika na wao hivyo hivyo. Watafutie muda muafaka ambao hutawaingilia na mambo yao. Usiwaite katikati ya muda ambapo michezo imekolea.
 Unaweza kutumia muda ule wanapotaka kula, au wakikutaka ucheze nao. Pata muda uwasomee. Wakati chakula kipo mezani, wakiwa wanakula, badala ya kuwaelekezea kwenye tv ili upate muda wakufanya mambo mengine, tenga hata dakika kumi tu, watafutie kitabu chenye hadithi nzuri, wasomee wawe wanakusikiliza wakati wao wanakula, na wakati mwingine kama kina picha, waonyeshe picha huku ukiwasomea. Inakuwa ni kama wanasikiliza radio wakati wanakula. Au unapomaliza shuguli zako, na unapokuwa nao karibu, pata muda wakucheza na watoto wako, wasomee hadithi huku ukiigiza sauti za wahusika wa kwenye kitabu hicho unacho wasomea. Kama ni simba, nguruma kama simba, kama ni nyoka, tambaa sakafuni kama nyoka ili kuwafurahisha na waone uzuri wa kile unachowasomea.



4. Usimlazimishe kwa hasira mtoto wako kujifunza kujisomea:-
Kusoma sio vita. Na hapa ndipo wazazi wengi 
tunapokesea. Tunatamani matokeo ya haraka, nakutaka mtoto afahamu au apende kwa haraka. Na wasipoonekana kufanya kile tunachoona ni sahihi kwao, tunakuwa wakali zaidi. Matokeo yake, tunawafanya wanakuwa adui wa kitu chema. Utakapoona bado hafurahii kujisomea mwenyewe, usimkasirie, au kumchapa na kumlazimisha. Endelea kuwasomea tu bila kuonyesha ni adhabu kwako au anakupotezea muda. Huku ukimuwekea aina ya vitabu anavyopenda kutokana na mtoto wako. 
Usimuwekee aina ya vitabu vya wanyama, wakati unajua anapenda magari. Tafuta vitabu ya vitu unavyoona anapenda kucheza mara kwa mara.
 Na hapo pia, tukumbuke wazazi lengo si mtoto kusoma vizuri. Lengo kubwa ni kumfanya mtoto apende vitabu. Usianze kulazimisha mtoto asome vizuri kwenye muda huo. Huo ni muda wa furaha, unaotaka aone kitabu ni rafiki. Wapo watoto 
wengine wanachelewa kusoma, na wengine wanawahi. Mpe muda mtoto wako, atakapofikia kipindi amependa vitabu, atalingana na hata yule mtoto aliyeanza kusoma akiwa na miaka minne. MPE MTOTO WAKO MUDA.

5. Tengeneza muda maalumu wa kusoma kila siku:-

Tengeneza muda mzuri unaojua unawafaa watoto wako kusoma, yaani wakiwa wametulia, wakiwa hawana mambo mengi yakufanya. Iwe jioni wakisubiria chakula, au wakati wametoka shule wakiwa wanapumzika, muda ambao hata wewe mwenyewe umetulia.  Huo ndiwe uwe muda wenu kila siku na wao wajue hivyo. usibadilike badilike. Yaani leo asubuhi, kesho mchana, au muda utakao jisikia wewe. Weka rutini. Wasomee watoto wako au wape vitabu kwa muda huo wasome, au wakuone na wewe umeshika kitabu unasoma, na wao wataiga kwako.

6. Waachie wakati mwingine mkubwa wao awasomee:-

Hii inafanya kazi vizuri kwenye familia yenye watoto zaidi ya mmoja. Wakati wote watoto hupenda kushindana. Mimi nilianza kwa kumpa dada yao awe anawasomea, huku nikiwepo karibu kusaidia kwa yale maneno magumu asiyoweza kuyasoma. Ndipo wadogo zake walipoona ni 
rahisi. Na wao wakataka kuwekwe zamu za kusoma, kwa kuwa walijua wanaposhindwa sio kosa, nipo kwa ajili ya kuwasaidia. 


7.Wanapoenda kulala, wawekee vitabu pembeni yao:-
Wape watoto wako muda fulani wakujisomea vitabu wanavyopenda kabla ya kulala, yaani wawapo kitandani. Kama ni familia mnazozima taa usiku, basi wape hata dakika 20 tu, na vitabu vyao kabla hujakwenda kuwazimia taa. Na kama wanalala na taa zikiwa zinawaka, wape muda, kuwa baada ya dakika fulani nitakuja kuwaambia mlale. Itawasaidia sana kupenda kusoma kwa 
sababu watoto wengi hawapendi kuwahi kulala, na endapo watajikuta na kitabu tu kitandani bila mchezo mwingine, itawalazimu kusoma ili asilale mapema, na ndipo utamkuta alishapitiwa na usingizi. Toa kitabu, muwekee pembeni, kwa ajili ya kesho yake.






8.Usibadili vitabu kwa haraka:-

Hii ni siri waliyonipa walimu wa watoto wangu.
Endapo ukigundua aina ya vitabu anavyo vifurahia mtoto wako, na ukakipata, msomee au mwache akisome mara kwa mara. Hata kama ni zaidi ya juma moja{Week}. Hii humsaidia kujifunza maneno magumu aliyokutana nayo kwenye kile kitabu. Na kuyaelewa, nakuweza kuyasoma wakati mwingine. Msaidie kwa kumwambia ayaandike, kama anaweza kuandika, ili kila anapokutana nayo wakati mwingine aweze
kuyatambua, na kama endapo wewe ndiye unayemsomea, jaribu kumuuliza maswali kama ameelewa hilo neno na jaribu kumpa tafasiri yake kwa mifano. Arudiapo kusoma kitabu kimoja mara kwa mara, kinamuongezea ujasiri wa kukisoma kwani anakuwa ameshajua stori ya kile kitabu.




HUJACHELEWA. 
HATA KAMA MTOTO AMEFIKIA UMRI MKUBWA, ANZA NAYE TARATIBU KWA KU{SUBSTITUTE}. KAMA NI MPENDA MICHEZO SANA, AU MUANGALIA TV SANA, MPUNGUZIE MUDA HUO, PATA MUDA WA KWENDA NAYE MAKTABA, AU MLETEE VITABU VYA VITU ANAVYOPENDA KUFANYA AU KUANGALIA. eg..KAMA ANAPENDA KUIMBA, TAFUTA VITABU VYENYE STORI ZA MZIKI AU WACHEZA MPIRA N.K

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.