Zitto Kabwe kujiuzulu ubunge tena



ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge pekee wa chama hicho ametangaza kujiuzulu ubunge wake iwapo serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), itathibitisha kuwa akiba ya chakula inayofikia tani milioni 1.5 Inayofikia tani milioni 1.5, 
Zitto ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini ametoa msimamo wa kujiuzulu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook na Twitter.
“Serikali ya CCM ikinionesha tani 1.5 milioni za chakula ambazo inataka kusambaza, najiuzulu Ubunge mara moja. Narudia, mpaka Oktoba 2016 kulikuwa na nafaka tani 90,400 tu kwenye maghala yote ya NFRA.
“Tunashukuru kuwa Hivi sasa ajenda ya tishio la njaa inapata majawabu na matamko. Ndio wajibu wa vyama vya siasa. Kuibua masuala muhimu kwa nchi yetu,” ameandika Zitto.

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli imekuwa ikisisitiza kuwa taifa halijakumbwa na njaa na hakuna chakula cha msaada ambacho serikali itakipeleka kwa wananchi, bali wananchi wafanye kazi kwa bidii ili kujipatia kipato halali.


Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo ya nchi, zimeripotiwa taarifa za kuwepo kwa uhaba wa chakula unaotokana na ukame kiasi cha kusababisha vifo vya mifugo kwa kukosa malisho.

Jana Waziri Mkuu Majaliwa Kassim aliwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa kuna akiba ya chakula inayofikia tani 1.5 milioni ambazo tayari wameruhusu zisambazwe katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuuzwa katika maeneo mbalimbali na kudhibiti kupanda kwa bei.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.