Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Mh. Mbowe alaani kitendo cha polisi kumkamata Mh.Lowassa.


Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe, amelaani kitendo cha jeshi la polisi mkoa wa Geita kumkamata mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho na waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa, wakati akielekea kata ya Nkome jimbo la Geita vijijini kushiriki mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.

Mh. Mbowe ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha kamati kuu ya chama hicho, kilichofanyika hii leo jijini Mwanza, ikiwa ni siku moja baada ya jeshi la polisi mkoani Geita kumkamata Mh. Edward Lowassa alipowasili mkoani humo akitokea mkoani Kagera alikokuwa kwa shughuli za kisiasa, akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wengine wa kamati kuu akiwemo Prof. Mwesigwa Baregu, baada ya mwanasiasa huyo kusimama kwa lengo la kuwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika barabarani.

Tukio hilo lililotokea jana majira ya saa 9.20 alasiri, na kusababisha jeshi la polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wakielekea katika kituo cha polisi cha wilaya ya Geita, ambako Mh. Lowassa na wenzake walitakiwa kuandika maelezo pamoja na kufanyiwa mahojiano na kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo linaelezewaje na mwenyekiti huyo wa Chadema Taifa Mh.Freeman Mbowe.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.