Vijana hao ambao majina yao hayakutambulika mara moja walijikuta matatani baada ya kuzingirwa na kukamatwa na wafanyabiashara hao ambao wanadai kuwa wamechoshwa na vitendo vya wizi kila kukicha ,huku wakidai kuwa askari polisi wa eneo hilo huwakamata na kuwaachia kwa madai ya kukosekana kwa Ushahidi.
Wakizungumza na Chanel ten baadhi ya wafanyabiashara hao wamedai kuchoshwa na vitendo vya wizi katika eneo hilo ingawa walisema hatua wanazochukua za kuwaadhibu ni kinyume cha sheria.
Wakati huo agizo la kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo katika barabara za mwendo kasi lililotolewa na waziri wa Tamisemi george simbachawene limeonekana kukwama kutokana na wafanyabiashara hao kuendelea kufanya biashara tena mbele ya kituo cha mabasi ya mwendo kasi gerezani na kusababisha usumbufu mkubwa eneo hilo.
Kwa matokeo ya kidato cha nne bofya hapa http://masengwa.blogspot.com/
