KAMPUNI kubwa ya magari nchini Marekani Ford, imetangaza kuachana na mpango wake wa kutaka kutengeneza kampuni ya magari nchini Mexico itakayogharimu dola bilioni 1.6 ili kuwekeza zaidi nchini Marekani.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ford, Mark Fields amesema maamuzi hayo ni matokeo ya kura ya Imani ya wanaounga mkono biashara iliyokuwa ikiundwa na Rais Mteule wa nchi hiyo, Donald Trump.
Mapema siku ya Jumanne ametoa tishio sawa na hilo kwa Kampuni ya General Motors.


