CCM yawataka watanzania kubeza watu wenye nia mbovu ya kukwamisha maendeleo

Image result for humphrey polepole

Chama cha Mapinduzi kimewataka watanzania kubeza watu wenye nia ovu ya kukwamisha juhudi za maendeleo zinazoletwa na serikali ya awamu ya tano kupitia chama cha Mapinduzi na badalayake waendelee kuungamkono chama hicho wakati wakufanyika mageuzi yanayolenga kuongeza demokrasia,uwajibikaji,vita dhidi ya rushwa pamoja na ubadhilifu wa mali za uma ili kuleta maendeleo ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na katibu mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM Humphrey Polepole jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari ikiwa ni siku chache baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Dimani huko Zanzibar pamoja na chaguzi 20 za kata mbalimbali hapa nchini ambapo amesema siri ya ushindi wa chaguzi hizo ambazo CCM waliibuka kidedea ni kutokana na chama kurejea katika misingi yake pamoja na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi chini ya rasi Dkt John Pombe Magufuli.

Aidha, katibu huyo amewashukuru watanzania kwa kuendelea kuiamini serikali inayoongozwa na rais Magufuli kupitia chama cha Mapinduzi huku akisisitiza kuwa katika kipindi ambacho chama kinazaliwa upya kitaendelea kuchagua viongozi watakao kuwa wanasikliliza kero za wananchi watakao wachagua pamoja na kuzifanyia kazi kwa haraka.