VIJANA 15 WA UMRI WA MIAKA 16 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke jijini Dsm limewatia mbaroni
Vijana 15 chini ya umri wa miaka 16 wanaojihusisha na makundi ya
kihalifu maarufu panya Road ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya Uporaji
katika maeneo ya Mbgala na kuwajeruhi wananchi kwa mapanga na Visu
nyakati za jioni ambapo mmoja ameuwawa na wananchi huku wawili wakiwa
mahututi katika hospitali ya muhimbili.
Aidha
Jeshi hilo pia limewatia mbaroni wazazi 11 wa watoto hao ambao
wameshindwa jukumu la kuwalea watoto wao ambao wajiingiza katika makundi
hayo ya panya road ambao watashitakiwa kwa makosa ya kushindwa kuwalea
na kuwasimamia watoto wao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke Giles Muroto akizungumza na
waandishi wa habari amesema vijana hao wengi wao wakiwa wadogo
wamekamatwa baada ya kufanya vitendo vya Uporaji na kujeruhi kwa mapanga
katika maeneo ya mbagala jijini dsm juzi jioni.
Aidha
Kamanda Muroto amesema wazazi 11 nao wanashikiriwa na jeshi hilo kwa
kushindwa kuwasimia watoto wao ambapo amesema kwa mujibu wa kifungu cha
sheria cha 14,Mzazi atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake atafikishwa
mahakamani na kufungwa jela miezi 6 au fani ya shilingi milion 5.
Baadhi
ya wazazi waliokuwapo katika kituo cha Polisi Chang’ombe wamesema wengi
wao walikuwa hawajui kuwa watoto wao wanajihusisha na makundi hayo
lakini baadhi ya watoto wamedai kuwa baadhi ya wenzao wamekuwa
wakikusanyika katika camp na kuwashawishi kushiriki katika vitendo hivyo
vya Uporaji.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi