JPM AMTEUA PROF. LAWRENCE MUJUNGU MUSERU KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
03 Oktoba, 2016 amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa
na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam
imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza jana
tarehe 02 Oktoba, 2016.
Kabla ya Uteuzi huo Prof. Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Oktoba, 2016
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi