KOCHA SIMBA ATAMBA KUPATA USHINDI DHIDI YA AL MASRY YA MISRI


FADLU Davids, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri.

Huo ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni hatua ya robo fainali na kwa sasa kikosi kipo Misri kwa maandalizi kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025.

Robo fainali ya kwanza Simba watakuwa ugenini na ile ya pili watakuwa Uwanja wa Mkapa Aprili 9 ambapo mshindi wa jumla kwenye mchezo huo atakata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Fadlu amesema kila hatua ni muhimu kupata ushindi kutokana na umuhimu wa mchezo hilo wanalitambua na wanalifanyia kazi kwenye eneo la uwanja wa mazoezi kuwa bora zaidi.

“Kazi ni kubwa kwenye kila mchezo hasa hatua hii ambayo tupo, tunahitaji kupata matokeo na ugenini kuna ushindani mkubwa ila tuna faida kwenye mchezo wetu ujao ambao tutacheza Uwanja wa Mkapa.

“Wachezaji wanapambana kwenye mechi zetu ambazo tunacheza kutafuta ushindi imekuwa hivyo ninawapa pongezi kutokana na kujituma kwa kila wakati.”

Post a Comment

0 Comments