DRC: ATAKAYESAIDIA KUKAMATWA KWA VIONGOZI WA M23 KULIPWA NA SERIKALI




Wizara inayoshughulikia masuala ya Haki nchini humo imesema kitita hicho cha fedha kitakabidhiwa kwa yeyote, atakayesaidia kukamatwa kwa Corneille Nangaa, Bertrand Bisimwa na Sultani Makenga.

Kinshasa, inasema yeyote akayetoa taarifa sahihi zitakazosaidia kukamatwa kwa viongozi hao watatu, ambao wote walifunguliwa mashtaka mwezi Agosti mwaka 2024 bila uwepo wao na kuhukumiwa kifo.

Nangaa ambaye ni Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya uchaguzi nchini DRC, hivi karibuni alionekana akiwahotubia wakaazi wa Bukavu na Goma, ni kiongozi wa chama cha River Congo Alliance (AFC) ambacho ni kitengo cha siasa cha waasi wa M 23.

Haya yanajiri wakati huu, waasi hao wakiendelea kudhibiti maeneo mbalimbali jimboni Kivu Kaskazini na Kusini, ambapo wataalam wa Umoja wa Mataifa katika ripoti yao, wanaeleza kuwa waasi hao wanaungwa mkono na wanajeshi 4,000 wa Rwanda, madai ambayo serikali jijini Kigali imeendelea kukanusha.

Post a Comment

Previous Post Next Post