Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT) Dayosisi kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Usharika wa Ebenzer Kanisa Kuu amewataka waumini wa Kanisa hilo kusameheana hususan katik kipindi hiki cha Kwaresma.
Hayo ameyasema katika mahubiri yake ya Jumatano ya majivu iliyofanyika siku ya leo Jumatano 5/3/2025 katika usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga.
“Wakati mwingi lazima utafakari , Mungu amekusamehe mangapi? Kama Bwana angehesabu maovu yetu ninani angesimama? ungesimama wapi wewe? Lakini Mungu amekusamehe. Kama Mungu amekusamehe unatakiwa kuwasamehe na wengine, unatakiwa kuwahurumia na wengine”
“Kipindi hiki cha Kwaresma kitupeleke msalabani kutafakari maisha yetu usitembee na mizigo ya watu, na wengine mpo hapa hamsalimiani , hamtaki hata kukaa karibu, mwingine amekaa masharika na mwingine magharibi ukitoka hapo nje ni spidi, Mungu saidia bodaboda asikupitie. Lakini hutaki hata kusalimiana na watu. Lakini ni mkristo, unasali jumuiya moja, kanisa moja taifa moja na wakati mwingine mpo Chama kimoja pia lakini hamtakli kusameheana.” Alisema Mkiramweni.
Pia aliongeza kuwa, “maisha haya tunapita, huyajui ya kesho, ni fumbo, kama umesamehewa, Mungu amekufutia deni lako ni wakati wako kuwasamehe ndugu zako, watangaziwe msamaha hata kama hawajakuomba waambie umewasamehe, umenikwaza sana, yaani kati ya watu walionikwaza ni pamoja na wewe.”
“Kusamehe ni uwezo na kuyafuta yote yale yaliyokuumiza bila wewe kuendelea kuyahifadhi tena na haimaanishi kwamba hujaumizwa, umeumizwa sawa lakini Je,yeye aliyewambwa msalabani kwa ajili yako aliyetemewa mate, aliyedharirishwa, aliyevuliwa nguo uchi ,yeye hakuangalia hayo, aibu alizopata kwa ajili yako yeye kama alitusamehe na mpaka leo anatusamehe”
“Na kuna wimbo unasema HATA SASA VILE VIDODNDA BADO ANAVYO NA ALAMA ZA MISUMARI BADO ANAZO maana yake mpaka leo ule msamaha bado unafanya kazi, ile sadaka inafanya kazi ni mbichi.”
“Yeye ametufia, ameingia gharama kubwa , kwanini wewe unasema yaani wewe sikusamehi na sitaki kukuona mbele ya macho yangu? Ni wakati wa kusameheana sio wakati tu wa kwaresma lakini pia hata katika maisha yako yote unatakiwa kuishi kwa kuwasamehe wengine”
Pia mchungaji Mkiramweni amewataka washarika kutokubeba watu katika mioyo yao kwani ni kujipa mizigo isiyo ya lazima.
“Usikae na vinyongo, usikae na watu kwenye moyo wako, usikae na watu kwenye nafsi yako, usiwahifadhi watu. Halafu wakati mwingine umewabeba watu ambao hata hawaelewi kinachoendelea na baadae utakapowaambia watashangaa ilikuwaje, wasamehe ili ubaki na mani moyoni mwako."