DEREVA ASAKWA KWA KUIBA MAFUTA YA THAMANI MIL. 77



Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro linamsaka dereva wa Lori la kusafirisha mafuta Lori la mafuta nchini Uganda

kama Abubakari Adam Mwichangwe, mkazi wa Dar Es Salaam kwa kosa la kula njama ya kuharibu gari na kuiba mafuta lita 35,700 yenye thamani ya Tsh 77,112,000/= mali ya kampuni ya ACER Logistics Limited.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo tukio hilo limetokea Machi 16, 2025 usiku akitokea Dar Es Salaam kupeleka mafuta Lubumbashi nchini DRC Congo, akiwa Morogoro alikula njama na watu wengine watatu ambao kwa pamoja waliiba kiasi cha lita 35,700 za Dizeli ambayo yalishushwa kwenye vituo vya mafuta mali ya Simba Oil

Baada ya tukio hilo dereva aliendesha gari tupu na alipofika kitongoji cha Msufini kijiji cha Msimba katika barabara kuu ya Mikumi - Iringa wilaya ya kipolisi Ruhembe (Kilosa) dereva aliendesha gari hilo na kuliingiza kwenye korongoni akitaka kuaminisha umma kuwa limepata ajali na baadaye kuliwasha moto akijaribu kuliteketeza, kabla moto haujakolea ndipo wasamaria wema walifanikiwa kuzima na kutoa taarifa polisi hivyo uchunguzi unaendelea chini ya jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali.

Chanzo - EastAfricaTV

Post a Comment

0 Comments