Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini kupitia CHADEMA Mh Godbless Lema , Amenukuliwa huko Twitter akipinga POLISI KUFANYA KAZI KWA MATAKWA YA SIMBACHAWENE .
Mh Lema anadai mpaka sasa mtoto wa Simbachawene aliyedaiwa kudharau vyombo vya dola angali anashikiliwa Selo , jambo ambalo Lema analitafsiri kama ni uvunjifu wa KATIBA YA NCHI NA SHERIA ZILIZOPO , amesikitishwa sana kwa Jeshi la Polisi kuifanyia kazi kauli ya Simbachawene badala ya PGO , Pamoja na Sirro kung'olewa lakini bado shida ziko palepale .
Ni kweli kwamba mtoto wa Simbachawene amekosea lakini Haki zake zinapaswa kulindwa , Kosa alilotenda lina dhamana , lakini hadi sasa bado yuko rumande kwa vile tu Polisi wanamsikiliza Simbachawene , Mtoto akishazaliwa ni Mali ya Nchi , Ndio maana huwezi kuua mwanao tukakuacha , ni lazima tukukamate
0 Comments