
Mbunge na Mwanasiasa Mkongwe kutoka jimbo la Makambako Mkoani Njombe Deo Sanga ametangaza kufunga Ndoa na mke wake Rosana Kapasi katika kanisa la RC Ilangamoto na kisha kuhamishia sherehe yao kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Amani uliopo mjini Makambako, ambapo ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa siku ya tarehe 14 Septemba, 2022.
Akiongea na wananchi katika mkutano wake wa hadhara, mbunge huyo amesema tayari marafiki zake wameshamchangia ng'ombe 16 kwa ajili ya kula siku ya harusi yake na amewaalika wananchi wote kushiriki tukio hilo ambalo yeye na mke wake hawakuwahi kufanya hapo kabla
Tags:
habari