Kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria chini ya usharika wa Makedonia uliopo Jimbo la Shinyanga, wamezindua rasmi shule ya Makedonia English Medium ambapo mgeni rasmi wa uzinduzi huo alikuwa ni Askofu Dr. Emmanuel Joseph Makala
Uzinduzi huo umefanyika katika ibada takatifu iliyoongozwa na Askofu wa kwanza wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Daktari Emmanuel Joseph Makala
Katika mahubiri yake Askofu Daktari Emmanuel Joseph Makala, amesema uendeshaji na utoaji wa huduma za kijamii kama elimu kwa jamii ni sehemu moja muhimu kwa kanisa la Mungu na ndio mambo muhimu tuliyoitiwa kuyafanya katika umoja wetu.
Katika risala yake mwenyekiti wa kamati ya kikosi kazi Bwana Shuma amesema mchakato wa kuanzisha shule hii ulianzishwa mwaka 2015 chini ya mchungaji Helman Gacha aliyeleta wazo la kuanzisha kituo Day Care center na wazo hilo lilipokelewa na kuanza kutekelezwa mara moja.
Baadae usharika uliamua kununua kiwanja kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo na kiwanja hicho kilipatikana maeneo ya Lubaga manispaa ya Shinyanga. Chini ya mchungaji Harlod Mkalo pamoja na mchungaji mwenza Mathias Masele waliamua kuongeza nguvu kazi ndani ya kamati ya kikosi kazi ili kuhakikisha mambo hayakwami
Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema wakati shule hiyo inaanzishwa rasmi ilianza ikiwa na wanafunzi wawili na walimu wawili na baada ya miezi mitatu idadi ya wanafunzi ilifikia 27.

Askofu Dr Emmanuel Joseph Makala akisoma maandiko wakati wa uzinduzi wa shule hiyo
Askofu Dr Emmanuel Joseph Makala,wakuu wa majimbo pamoja na wachungaji wakiendelea na ibada ya uzinduzi wa shule
Askofu Dr Emmanuel Joseph Makala akijiandaa na ufunguzi
Baada ya uzinduzi na uwekaji wakfu wa Shule ya Makedonia English medium
Askofu Dr Emmanuel Joseph Makala akiendelea na ufunguaji wa majengo ya shule hiyo

Gari la shule ya Makedonia English Medium katika ubora wake
Hii ndio gari ya shule ya Makedonia English Medium kwa ajili ya wanafunzi
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Makedonia English Medium

Mwonekano wa majengo ya shule ya Makedonia English Medium

Picha zote na;
Isaac L. Masengwa
MASENGWA BLOG
Tags:
habari