
MSANII wa Bongo movie, Wema Sepetu ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Yanga amesema kufungwa kwao na Simba kulimfanya akose raha kutokana na kelele za watani wao hao wa jadi.
Aidha alisema wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia yatakapoanza atashabikia England kutokana na kuipenda kwake Manchester United inayotoka nchini humo.
Wema ambaye pia ni balozi wa Startimes, ameoneka kukerwa na mashabiki wa Simba kwa kusema tatizo ukame wa mataji umekuwa ukiwasambua kwa kipindi kirefu.
"Hatuna maneno mengi kama ilivyo kwa wenzetu wa upande wa pili, hayo wanayongea utadhani ndio wamechukua ubingwa na hata kama wakichukua mbona tumefululiza mara kadhaa na hatuchongi, " alisema na kucheka msanii huyo.
Hata hivyo, Wema alishukuru fursa aliyopewa ya kuwa balozi wa Startimes ambao watarusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi zote 64 za Kombe la Dunia kutoka nchini Russia kwa lugha ya Kiswahili.
Pia msanii huyo alisema pamoja na kuwa Mwafrika lakini kwenye mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kutimua vumbi Juni 14 hadi Julai 15, atashabikia England kutokana na kuipenda kwake Manchester United inayotoka nchini humo.
Naye Meneja masoko wa kampuni hiyo, David Malisa alisema jana kwenye ufunguzi rasmi wa msimu huu wa kombe la Dunia kuwa wamekuja kivingine hivyo Watanzania wategemee mazuri kutoka kwao