MAMBO YAIVA SIMBA... OKWI NA BOCCO WASISITIZA JAMBO MOJA TU


Kama kuna jambo wanalitamani mastaa wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi na John Bocco ni kutangazia ubingwa kwa Singida United, katika mechi itakayopigwa wikiendi ya wiki hii, kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.

Kinara wa ufungaji wa Ligi Kuu, Okwi mwenye mabao 20, amesema wakifanikiwa kupata pointi tatu ugenini basi ubingwa wao msimu huu utakuwa wa kihistoria.

Alisema anatamani ubingwa wautangazie katika ardhi ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua, kwamba wapinzani wao wana ubora wakiwafunga itadhihirisha uwezo walionao kwa msimu huu.

"Singida United ni timu ilioonyesha ushindani wa hali ya juu na siyo ya kubeza, tukiwafunga thamani yetu utapanda zaidi ya hapa tulipo, hilo ndilo jambo natamani litokee,"alisema Okwi.

Wakati mahesabu ya Bocco ni kuifunga Singida United ili michezo miwili itakayobakia iwe ni kwa ajili ya kutimiza ratiba kwa msimu huu.

"Sina maana tukifanikiwa kuwafunga Singida United, tutakuwa tumemaliza kazi, ila tunataka kumaliza biashara mapema, kitakachokuwa kimebakia ni burudani tu.

"Kitu kingine kinachonifanya nitamani tumalize kila kitu Singida ni kujitenga na wapinzani wetu wanaotufuata nyuma kwa nafasi ili wabaki kupambana wenyewe kwa wenyewe," alisema Bocco.

Post a Comment

Previous Post Next Post