
Uamuzi wa Azam FC, kuwaachia nyota wake Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aishi Manula na John Bocco ni moja ya sababu ya Simba kunyakuwa ubingwa msimu huu.
Nyota hao wamekuwa nguzo katika kikosi cha kwanza cha Simba huku wakiacha pengo mkubwa kwa Azam FC ambayo tayari imepoteza ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na Kombe la FA huku katika ligi ikigombea nafasi ya pili na Yanga.
Mabao 14 ya Bocco yamekuwa na mchango mkubwa kwa Simba msimu huu huku Azam ikiwa na ukame wa mabao.
Beki Nyoni, Kapombe wenye wamekuwa wakiipa Simba wingo mpana wa kutumia kila eneo linaloonyesha upungufu kutokana na uwezo wao wa kucheza namba nyingi uwanjani.
Kipa Manula amekuwa ni nguzo kubwa langoni mwa Simba akidaka karibu mechi zote na ameruhusu mabao 13 tu hadi sasa akiwa kipa aliyefungwa magoli machache.
Nyota hao waliondoka kwa pamoja ndani ya kikosi cha Azam FC msimu huu wakati huo kikiwa na mpango wa kuendeleza vipaji vya chipukizi zaidi.
Tags:
michezo