SARE YA SIMBA DHIDI YA STAND UNITED YAMTESA KOCHA SIMBA

Baada ya kulazimishwa sare ya 3-3 na Stand Utd, kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema hawakuwa na bahati katika mchezo huo.

Kocha Djuma alisema walikuwa na kila sababu ya kushinda mchezo huo, lakini walikuwa wanaruhusu mabao na kufanya mchezo kumalizika kwa sare.

"Tulikuwa tumewatangulia, lakini wao pia walikuwa wanafunga, tulipaswa kushinda kabisa lakini inawezekana bahati haikuwa yetu siku ya leo," alisema Mrundi huyo.

Akizungumzia kukosekana kwa wachezaji John Bocco na Emmanuel Okwi, alisema wachezaji hao wamekosekana baada ya kusumbuliwa na majeruhi.

"Ligi ndio kitu bora kwetu hivyo hatuwezi kuacha kumpanga mtu mwenye muhimu kisa mashindano makubwa, hawajakuepo kwasababu wanasumbuliwa na majeraha," alisema.

Naye kocha msaidizi wa Stand, Athuman Bilal 'Bilo', alisema walishaijua Simba ubovu wao upo wapi, hivyo walikuwa na kila sababu ya kupata bao.

"Simba udhaifu wao tuliuona kabla ya mechi kwahiyo sisi tuliingia huku tukiwa tunajua nini tunaenda kukifanya, pointi moja kwetu ina maana," alisema Bilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post