
Mshambuliaji mahiri wa klabu ya simba na mchezaji pekee anayeongoza kwa kufunga magoli mengi ligi kuu Tanzania bara Emmanuel Okwi amezungumzia matokeo ya jana baada ya simba kutoka sare na Stand united katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.
Okwi amesema timu ya stand united ni timu nzuri na sio timu ya kubeza kama wengine wanavyodhani.
"Stand United ni timu nzuri na sio ya kubeza kama wengine wanavyodhani. Ni timu ambayo ina wachezaji wazuri na siku zote mpira ni dakika tisini"
Alipoulizwa kuhusu kukosekana kwake kwenye mechi hiyo kuwa kunaweza kuwa kumesababisha simba kushindwa kuibuka kidedea katika mcheo huo Okwi alikanusha na kusema kuwa;
"Simba ilikuwepo kabla ya Okwi na ilishafanya vizuri zaidi ya sasa na ni timu yenye wachezaji wengi wazuri hata kikosi cha leo kilikuwa kizuri na wala hapakuwa na shaka na pengine nami ningecheza mchezo wa leo tungefungwa zaidi"
Jana Simba ililazimishwa sare ya 3-3 dhidi ya Stand united katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Tags:
michezo