DK 50 Raphael Daud yuko chini pale akimlalamikia mwamuzi namna alivyoangushwa. Anatolewa nje kwenda kutibiwa
GOOOOOOOOO Dk 46, Kapama anaukwamisha mpira wavuni akiunganisha pasi safi kabisa ya Ngassa
Dk 45 Mechi inaanza kwa kasi Ndanda wakionekana wanataka bao la mapema ili kuwapa Yanga presha
DAKIKA 2 ZA NYONGEZADk 45, Abdallah naye anaachia mkwaju lakini hakulenga lango
Dk 44, Majogoro naye anaachia mkwaju hapa lakini hakulenga lango
Dk 42, krosi nzuri ndani ya lango la Ndanda, Kisubi anatokea na kudaka vizuri kabisa hapa
SUB Dk 40 Waziri Majogoro anaingia kuchukua nafasi ta Baraka upande wa Ndanda
Dk 40, anakwenda kupiga Tshishimbi, kipa anadaka na kuuficha kabisa
GOOOOOOOOOOOOO Dk 39 KADI 37 John George analambwa kadi ya njano PENAAAAAAAAAAAAAAT Dk 36, Yanga wanapata penalti baada ya beki wa Zabron kuunawa
Dk 34, Yanga wanachofanya ni kuupoza mpira wakisikilizia mabao yao mawili lakini wanashambulia kwa kushtukiza kila wanapopata nafasi
Dk 32, Martib anaingia vizuri lakini anaanguka na kipa anauwahi mpira
GOOOOOOOOO Dk 29 Kessy anachambua kama karanga kabla ya kuandika bao saaaafi la pili
DK 28, pasi ya Buswita, Martin anajaribu lakini ni shuti mtoto
Dk 25 Yanga wanalazimika kumuweka chini Ngassa, lakini mpira faulo naye anapiga nyanya kabisa na Rostand kama maji anadaka
Dk 23 nafasi nzuri nyingine kwa Yanga, kipa anaugusa, Ndanda wanaokoa
Dk 20, kona maridadi ndani ya lango la Ndanda, kipa Kisubi, anatoka na kuupiga ngumi
Dk 20, Ajibu anaachia mkwaju matata kabisa lakini kipa anaokoa kwa umaridadi kabisa. Kona
Dk 19, Ndanda wanapata kona, inachongwa lakini Yondani anaruka na kuokoa
Dk 19, inachongwa faulo vizuri na Ajibu, inaokolewa vizuri
Dk 18, Yanga inapata adhabu nje kidogo ya eneo la Ndanda
DK 15, Ndanda wanafanya shambulizi kali lakini mpira wa shuti la tik taka, unaishia mikononi mwa Rostande
Dk 13, inaonekana kuna makosa mengi sana katika difensi ya Ndanda na wanapaswa kuwa makini
Dk 10 shuti kali katika lango la Yanga, safari hii kipa yuko makini anaokoa, unamtoka anadaka tena
Dk 8, kona nyingi ya Ndanda, lakini Yanga wako makini wanaokoa hapa
Dk 7, Ndanda wanapata kona, inachongwa hapa, Rostand anaokoa na kuwa kona tena
GOOOOOOOO Dk 6, Buswita anafunga kwa ulaiiiini baada ya uzembe wa kipa na mabeki.
Dk 4, Ngassa tena anaingia vizuri, anapiga shuti la chinichini, goal kick
Dk 3, Ngassa anaachia mkwaju mkali, nusura afunge lakini hakuwa makini
Dk 1 Ndanda FC ndiyo wanaanza kushambulia kwa kasi