HAJI MANARA ATUMA SALAAM ZA IJUMAA KWA MASHABIKI WA SIMBA

Simba imefikisha pointi 42 huku ikiwa kileleni na ikifuatiwa kwa ukaribu na wapinzani wao Yanga wenye tofauti ya pointi 5. 

Dar es Salaam. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametuma salamu za Ijumaa 

kupitia ukurasa wake wa Istagram baada ya matokeo ya jana Simba iliyopata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mwadui. 

Manara alisema mengi yamesemwa kwamba Simba imeanza kuyumba, lakini akafafanua kwamba kauli hizo zinatoka kwa wapinzani wao ambao wanaamini kuwa Mungu ni wao peke yao. 

Kiongozi huyo machachari wa Simba alisisitiza kwamba mashabiki wa timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi wapuuzeni kauli za kuwavunja moyo.
Alisema kwamba wao kutoka sare sio jambo la ajabu kwani Mwadui imezifunga Singida United kabla ya mchezo wa jana Alhamisi, pia waliwafunga Mtibwa 3-1 Shinyanga na waliwahi kutokoka sare na Yanga na Azam tena wakiwa Dar es Salaam 

Manara alihoji kwamba kwanini wao kutoka nao sare na Mwadui ndiyo iwe nongwa tena ugenini?

Alisema Simba haitatoka kwenye mstari na washabiki watulieni na wazidi kuiombea timu na kuisapoti huku akisema kwamba bado wanaongoza ligi. 

Manara alitia kijembe akisema kwamba “Msisahau Mwadui hawa hawa walisababisha Boniface Mkwasa kunusurika kupigwa na washabiki wa Yanga baada ya kutoka nao sare.”

Post a Comment

Previous Post Next Post