Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.
Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.
Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.
Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.
Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Novemba, 2017 amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Mhe. Samia Suluhu Hassan amemfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake.
Mhe. Tundu Lissu amemshukuru Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao.
“Msalimu Mhe. Rais mwambie namshukuru sana kwa salamu zake na kunijulia hali” amesema Mhe. Tundu Lissu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana walipofika hospitalini hapo kumjulia hali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika hospitalini hapo kumjulia hali.
BONYEZA HAPA CHINI UANGALIE VIDEO YAKE
CHANZO- MICHUZI
Tags:
habari