
WACHEZAJI wa Yanga, wamepewa mapumziko ya wiki moja kwenda kula 'bata' na familia zao na watarudi uwanjani Jumatatu hii.
Yanga inayonolewa na kocha Mzambia, George Lwandamina imewaruhusu wachezaji wake kwenda katika mapumziko hayo kutokana na kusimama kwa mechi za Ligi Kuu Bara.
Ligi Kuu imesimama kwa ajili ya kupisha mashindano ya Kombe la Chalenji yanayotarajiwa kuanza wikiendi hii nchini Kenya.
Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema: "Mazoezi yataanza rasmi Jumatatu ijayo, tumewapa mapumziko wachezaji wetu mpaka siku hiyo. Mapumziko hayo ni kwa sababu hatuna mechi kwa siku za hivi karibuni."
Wachezaji wa Yanga wanaounda kikosi cha Kilimanjaro Stars kinachoiwakilisha Tanzania Bara ni Gadiel
Michael, Kevin Yondan'Vidic', Rafael Daudi na Ibrahim Ajib.
Hata hivyo, watani wao wa jadi Simba, wao wamewapa wachezaji wao mapumziko ya siku nne na watarudi uwanjani Ijumaa hii.
Tags:
michezo