
Mwenyekiti wa Stand United Ellyson Maeja akiongea kwa Kujiamini jana alisema kuwa Simba lazima afe kwa bao 2 siku ya Jumapili, Maeja amesema Simba wameanza Kutapatapa mapema kwani hawajataka Kukaa Shinyanga wakiwahofia.
Maeja amesema
"Kuna Raha kumfunga Simba, Lazima Simba tumfunge bao 2 Kwanza Tunacheza nyumbani lakini pia tumeshatoa Nuksi ya kutoshinda kwenye Ligi kwa kumfunga Mbeya City kwahiyo Simba Tutamfunga BAO 2".
Simba walio nafasi ya 4 kwenye Msimamo wakiwa na Points 8 baada ya Kushinda mechi 2 na sare 2 imekuwa ikipata matokeo kwa taabu katika uwanja huo wa CCM KAMBARAGE.
Tags:
michezo