AZAM WAUPONDA UWANJA WA JAMHURI DODOMA, WAZUNGUMZIA MAJERUHI

Kuelekea Mchezo kati ya Singida United na Azam Fc, Azam Fc kupitia kwa Afisa Habari wake Jaffar Iddi wamesema Uwanja wa Jamhuri Dodoma hauna matunzo, Haumwangiliwi maji na leo wanaenda Kucheza kama Kwenye Udongo tu.

Jaffar Iddi amesema pia Mchezaji Steve Kingwe ameumia wakiwa mazoezini walipokuwa wakifanya mazoezi katika uwanja wa UDOM kwahiyo mchezaji huyo ataukosa Mchezo wa Leo dhidi ya Singida United.

Azam wapo nafasi ya Pili wakiwa na point 10, na Singida Nafasi ya tatu wakiwa na Points 9 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo minne.
Previous Post Next Post