KAULI YA SIMBA YAWAPA RAHA MASHABIKI WAKE, YAONESHA TIMU IKO IMAR

Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Klabu ya Simba ametoa kauli ya Kujiamini kuelekea pambano kati ya Yanga na Simba Oktoba 28 akisisitiza kuwa Simba wako tayari kucheza na Yanga uwanja wowote.

Tuko tayari kucheza uwanja wowote ambao utakuwa umepangwa maana yake sisi tunakuwa wenyeji,Tumeenda Chamazi bado sisi washabiki wetu walikuwa wengi kuliko Azam,lakini pia tumekuja Kucheza Mwanza tulikuwa na washabiki wengi kuliko Mbao.

Tully ameenda Mbali zaidi na Kusema wako tayari kucheza hata Nje ya Tanzania maana wameiandaa timu yao Vyema.

Simba kama klabu tumejiandaa kucheza kiwanja chochote ambacho kipo ndani ya Tanzania na Ikiwezekana hata nje ya Tanzania, kwamaana tumeiandaa timu yetu kucheza na timu yoyote na kucheza Sehemu yoyote.

Juzi kati kuliibuka taarifa za Yanga kutaka kutumia uwanja wa CCM KIRUMBA kwenye pambano lao dhidi ya Yanga hata hivyo taarifa hizo hazijathibitishwa na Uongozi wa Yanga.
Previous Post Next Post