
Moja kati ya wajumbe wa Kamati ya Masoko ndani ya Klabu ya Yanga Vincent Kigosi(RAY) ameliambia gazeti hili kuwa kamati yake Kupitia Kundi linalojulikana kama Yanga Forever wamejipanga kuwa wanatoa zawadi ya shilingi laki 5 kwa mchezaji bora wa Kila mechi.
Zawadi ya Kwanza imedondoka kwa mchezaji Kelvin Yondani ambaye alifanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya Ndanda KWANI kulingana na maelezo ya Ray Mchezaji Yondani alicheza vizuri nafasi ya Ulinzi kama beki wa Kati lakini pia alitoa pasi ya Goli (Assist).
Ray amesema mchezaji bora wa kila mechi atakuwa akichaguliwa na jopo la Wataalamu na kisha wao watakuwa wanaangalia kama kweli anastahili kisha anapewa mzigo wake wa Shilingi laki Tano.
Kamati ya Masoko wameamua kufanya hivi ili kuhakikisha kila mchezaji anapambana na kuisaidia timu kupata ushindi.
Tags:
michezo