
USAJILI YANGA LEO JUMAMOSI 29 JULY 2017 (29.7.2017)
Klabu ya Yanga Kupitia Kwa Afisa Habari wake Dismas Ten Imeweka wazi juu ya Mustakabari wa Wachezaji wawili wa Kigeni wanaoonekana kwenye mazoezi ya Yanga lakini Uongozi haujatoa neno Lolote kama wamesajiliwa ama bado.
Dismas Ten amesema wachezaji hao Mmoja raia kutoka Ghana Tony Okoh na Mwingine kutoka Cameron Fernando Bongnyang Wachezaji hao wapo katika Majaribio na uamuzi wa kusajiliwa au Kutosajiliwa Upo chini ya kocha George Lwandamina.
Endapo George Lwandamina atakubali Juu ya uwezo wao basi Atachonga na Kamati ya Usajili ili kuweza Kumalizana kwenye masuala ya usajili.
Wachezaji hao ni moja kati ya wachezaji waliopo kwenye kambi ya Morogoro wakila dozi ya Mbili kwa Siku.
Tags:
michezo