VIDEO: TAARIFA YA KAMATI YA BUNGE BAADA YA KUMHOJI RC MAKONDA

Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika amesema kuwa kamati hiyo imefanya mahojiano na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana mkoani Dodoma kufuatia agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa kiongozi huyo wa mkoa ameonyesha ushirikiano katika mahojiano hayo na kuwa ripoti itafikishwa kwa Spika wa Bunge kwa ajili ya hatua zaidi.

Makonda amehojiwa kufuatia kauli yake aliyoitoa kupitia kituo cha runinga kuwa wabunge wanapiga porojo na kusinzia tu kitu ambacho kilitafsiriwa kama kashfa na kulidharau Bunge.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO YA TAARIFA HIYO






Previous Post Next Post