RAISI MAGUFULI AUNDA KAMATI YA KUCHUNGUZA MCHANGA WA MADINI ULIOKAMATWA BANDARINI


Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ameteua kamati ya wataalamu watakaofanya uchunguzi kwa lengo la kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena yenye mchanga wa madini yanayoshikiliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini. 
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kamati hiyo yenye wajumbe 8, inatakiwa kuanza kazi haraka iwezekanavyo. 

Wajumbe wa Kamati hiyo ni; 


Prof. Abdulrahman Hamis Mruma
Prof. Justianian Rwezaura Ikingula
Prof. Joseph Bushweshaiga
Dkt. Yusuf Ngenya
Dkt. Joseph Yoweza Philip
Dkt. Ambrose Itika
Mohamed Zengo Makongoro
Hery Issa Gombela
Wajumbe wote wa kamati hii wanatakiwa kufika ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 31 Machi, 2017 saa 4:00 asubuhi.
Previous Post Next Post