
Mtoto, Mgulumi Saning'o (11), mkazi wa Kijiji cha Kongogo Kata ya Babayu wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma, amekatwa mkono wa kulia baada ya kujeruhiwa na waya wa umeme uliokuwa uliokuwa unaning'inia eneo la kijiji hicho.
Mbali na kupoteza mkono, mtoto huyo ameungua sehemu mbalimbali za mwili kuanzia miguuni hadi mikononi baada ya kupigwa shoti ya umeme katika tukio lililotokea Mei 4, 2026.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Mei 31, 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, baba wa mtoto huyo, Mlewa Saning'o amesema ajali hiyo ilitokea wakati mtoto wake alipokuwa akicheza pamoja na wenzake karibu na eneo ambalo waya huo ulikuwa ukining’inia.
Amesema mtoto huyo alipokuwa akipita eneo hilo aligusa waya wa umeme uliokuwa unaning'inia kwenye nguzo na kupigwa shoti iliyomsababishia majeraha makubwa.
Chanzo: MWANANCHI
0 Comments