MIGODI YA BARRICK TANZANIA YAFIKISHA ELIMU YA USALAMA KWENYE JAMII MAONESHO YA OSHA NJOMBE


Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Mhe. Anthony Mtaka akipokea moja ya mitungi ya gesi uliotolewa na Barrick
Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Mhe. Anthony Mtaka akipokea Zawadi ya begi kutoka Afisa Mifumo ya Usalama wa Barrick, Beatrice Amos.
Afisa wa Usalama kutoka Mgodi wa Barrick Mgodi North Mara, Maisori Mniko akizima moto kwa vitendo katika mafunzo ya siku moja ya kupambana na majanga ya moto.
Afisa Msimamizi wa Usalama kutoka Barrick North Mara, Athanas Mtenga akitoa elimu ya usalama mahala pa kazi kwa wajasiriamali wa Mkoani wa Njombe.
Baadhi ya timu ya wafanyakazi wa Barrick kwenye maonesho
Majaji wa OSHA wakipita katika banda la maonesho la Barrick.

***
Elimu ya afya na usalama mahali pa kazi inaendelea kuwafikia wananchi mbalimbali ambao wanatembelea banda la maonesho ya kampuni ya dhahabu ya Barrick kupitia migodi yake ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi kwenye maonesho ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) yanayoendelea mkoani Njombe.

Mbali na elimu hiyo pia wafanyakazi wa Barrick wameshiriki katika programu za kutoa elimu ya afya , usalama na udhibiti wa majanga ya moto kwa makundi mbalimbali mjini Njombe kwenda na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo Mazingira bora ya kazi kisaikolojia ni njia ya kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na kujenga taasisi imara.

Afisa wa Barrick North Mara , Kitengo cha Dharura na Uokoaji , Maisori Mniko ameeleza kuwa mbali na kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda la Barrick mwaka huu wataalamu wa masuala ya usalama wamefikisha elimu ya usalama kwenye makundi mbalimbali nje ya eneo la maonesho ikiwemo mama lishe,madereva wa bodaboda na vikundi vya ujasiriamali vya Wanawake.

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa wajasiriamali wa Njombe kujifunza jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto.

Amesema mwitikio wa wananchi kupokea mafunzo ya usalama umekuwa ni mkubwa na wengi wao wameuliza maswali mbalimbali kwa wataalamu wa usalama kutoka Barrick ni jinsi gani ya kukabiliana na majanga ya moto na ajali nyinginezo.

Barrick imekuwa ikitekeleza kampeni ya ‘Journey to zero’ ambayo inalenga kuhamasisha afya na usalama kwa wafanyakazi wake ambayo sasa inapelekwa kwa wadau wengine wote kwenye jamii.

“Kampeni yetu ya 'Journey to Zero' inalenga kuhakikisha wafanyakazi wote wa kampuni wanakuwa salama wakati wote wanapokuwa kazini hadi wanaporudi nyumbani hivyo tumehakikisha kampeni hii inavuka mipaka hadi nje ya kampuni kuhakikisha jamii nzima inakuwa salama na ndio maana tunaendelea kuendesha mafunzo ya usalama kwa jamii ili kuhakikisha jamii yote inakuwa salama”, amesema.

Mmoja ya wanufaika wa mafunzo hayo , Mariam Hongoli, kutoka Makambako , amesema kwamba ni muhimu kwa wakazi wa Njombe na vitongoji vyake kujifunza mambo ya kukabiliana na ajali kama vile za moto kwa maslahi mapana ya familia na jamii kwa ujumla.

“Mafunzo haya ni muhimu kwa sababu hata ukiwa nyumbani na watoto unaweza kukabiliana na majanga kama ya moto kwa ufanisi na kuuzima baada ya kupata elimu hii,” amesema Hongoli.

Wakati huo huo banda la maonesho la Barrick limekuwa likitembelewa na viongozi mbalimbali na Serikali na wananchi ambao wameweza kuona vifaa mbalimbali vya kisasa vya usalama na udhibiti wa majanga mbalimbali ikiwemo moto pia kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa usalama.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Juma Sweda ni miongoni mwa wageni waliotembelea banda la Barrick katika maonesho hayo na kupongeza kampuni kwa kuwekeza katika vifaa vya usalama vya teknolojia ya kisasa sambamba na kuwa na programu za kutoa elimu ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi kwenye jamii nje ya migodi yake.

Usalama ni sehemu muhimu ya DNA ya Barrick. Katika kudhihirisha hilo migodi yake nchini imekuwa ikishinda tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi za nchini na za nje.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Mhe. Anthony Mtaka akipokea zawadi ya begi kutoka Afisa Mifumo ya Usalama wa Barrick, Beatrice Amos.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe akipokea moja ya mtungi wa gesi ulitolewa na Barrick kwa ajili ya kusaidia wajasiriamali.
Afisa Usalama wa Barrick North Mara , Maisori Mniko akitoa mafunzo jinsi ya kuzima moto kwenye mafunzo yaliyoendeshwa na Mgodi wa Barrick North Mara


Wajasiriamali kutoka Mkoa wa Njombe na vitongoji vyake wakiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi na maafisa usalama kutoka Migodi wa Barrick.

Post a Comment

0 Comments