BARRICK YATOA SHILINGI 25 BILIONI KWA UDSM ILI KUWEZESHA TAFITI , UFADHILI , KUONGEZA RASILIAMALI WATU KWENYE SEKTA YA MADINI NCHINI

 

Meneja Mkazi wa Barrick Nchini , Dkt. Melkiory Ngido (kushoto) akibadilishana mkataba wa ushirikiano na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) , Professor William Anangisye (Kulia). 
Meneja Mkazi wa Barrick nchini , Dkt. Melkiory Ngido (aliyekaa kushoto) akisaini mkataba wa makubaliano na ushirikiano na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) , Profesa William Anangisye (Kulia).
Meneja Mkazi wa Barrick Nchini Dkt. Melkiory Ngido na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) , Profesa William Anangisye wakionyesha mikataba ya makubaliano wa taasisi hizo mbili.
Meneja Mkazi wa Barrick Nchini , Dkt. Melkiory Ngido akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya 11 ya utafiti na ubunifu ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na Barrick kuingia makubaliano ya ushirikiano na chuo hicho.
Waziri Madini , Anthony Mavunde ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ya 11 ya utafiti na ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akizungumza kwenye hafla hiyo.
Waziri Madini , Anthony Mavunde ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ya 11 ya utafiti na ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akizungumza kwenye hafla hiyo
Mgeni rasmi Waziri Madini , Anthony Mavunde na Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiwa na Meneja Mkazi wa Barrick nchini , Dkt Melkiory Ngido kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Barrick nchini.
Waziri Madini , Anthony Mavunde akiwa na Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dk.Melkiory Ngido na makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye wakitembelea maonesho ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Barrick ni mdhamini Mkuu wa maonyesho hayo.
Kampuni ya Barrick nchini ambayo inaendesha shughuli zake kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals imeingia makubaliano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wa kuwajengea uwezo wanafunzi , wanataaluma na uwezeshaji tafiti mbalimbali hususani zinazohusu ukuzaji wa tasnia ya madini ambapo imetoa shilingi bilioni 25.

Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo (Mou) yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa maadhimisho ya 11 ya utafiti na ubunifu ambayo Barrick ni mdhamini mkuu , Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido amesema makubaliano hayo ni ya kipindi cha miaka 10 na yamelenga kuleta tija na ufanisi katika kukuza tasnia ya madini nchini kwa kuongeza tafiti, wataalamu nguvu kazi, ubunifu na kwa ajili ya kujenga uwezo kwenye tasnia kwa wanafunzi wa shahada , shahada ya uzamili na uzamivu.

“Tangu 2020 baada ya Twiga Minerals kuundwa Barrick imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuendeleza sekta ya madini ili iweze kuleta tija na maendeleo endelevu kwa nchini yetu,” amesema Dkt. Ngido.

Dkt. Ngido amesema kutokana na uhai wa migodi yake kuongezeka hadi miaka 25 mbele,Barrick itaendelea kushirikiana na Serikali katika jitahada za kuhakikisha sekta ya madini inafanikisha kuleta mapinduzi ya uchumi nchini.

Pia alisisitiza makubaliano yana lengo la kuongeza uelewa na ujuzi kwenye fani ya uhandisi wa madini , uchechuaji , biashara na sheria kwenye sekta hiyo ili kuweza kukuza mtaji wa rasiliamali watu kwenye sekta ya madini na Jiolojia nchini Tanzania.

Amefafanua kwamba Kampuni ya Barrick imetoa fedha hizo baada ya kuona umuhimu wa kuendelea kuwekeza kwenye tafiti, ubunifu kwa sababu ya mahitaji ya rasiliamali watu kutokana na ukuaji wa kasi wa tasnia ya madini nchini na maisha ya migodi kuhusishwa zaidi.

Amesema mradi huu utatoa fursa kwa wanataaluma zaidi ya 150 kufanya tafiti kwenye maeneo mbalimbali ya sekta ya madini ili kuja na mapendekezo jinsi ya kuandika sera, kanuni na sheria mbalimbali kwa lengo la kukuza sekta ya madini pia utanufaisha ufadhili wa wanafunzi zaidi ya 500.

Ameongeza kuwa sekta ya madini inahitaji ushirikiano kwa pamoja wa wadau wote ikiwemo UDSM hasa kwenye mradi huo wa miaka kumi ambao pamoja na mambo mengine itajenga uwezo, uelewa wa mambo ya kiufundi kitaalam, madini biashara , uhandisi wa madini na zaidi kujikita kwenye tafiti zenye tija.

Kwa upande wa Waziri wa Madini , Mh.Anthony Mavunde akizindua monesho hayo amesema nafasi ya wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwenye sekta ya madini katika kujenga uelewa , kukuza maarifa na ujuzi kwa manufaa na ustawi wa nchini ni kubwa kwa maslahi ya nchini kwa ujumla.

Ameongeza kwamba Tanzania ina ekari 233 millioni ila ni kilomita za mraba 945,000 tu ambazo tayari zimepiwa na kwa utafiti wa Kijioloji ani asilimia 97% (Geological mapping).

Amefafanua kuwa sekta ya madini inazidi kupiga hatua kubwa kwenye uchangiaji wa maendeleo ya nchini kama vile fedha za kigeni ni asilimia 56% na kuchangia kiasi cha shilingi trilioni 2.1 ambayo sawa asilimia 15% ya mapato yote ya ndani.

Waziri Mavunde amesema ni muhimu tuendelee kuwekeza kwenye tafiti ili kuweza kupata maeneo mapya yenye madini kwa ajili ya kupanua wigo wa uwekezaji wa nje na wa ndani kwenye sekta ya madini.

Katika mradi huo wa miaka 10 ni moja ya juhudi za kujenga maarifa, kukuza ujuzi katika sekta ya madini ili kuchochea ustawi wa jamii na nchini.

Ameongeza kuwa ni muhimu tuendelee kama taifa kuwekeza kwenye tafiti za kisayansi ili tuweze kupata nafasi ya kujua akiba ya rasiliamali za madini nchini nzima kwa kufanya upimaji wa kitaaluma wa ardhi yote ya nchini.

“Tukifanya utafiti wa ardhi yote ambazo tunazo kama nchini tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwa kuongeza thamani ya eneo letu na maisha ya watanzania kwa ujumla,” amesema Mavunde.

Ameeleza kuwa, kwenye uchangiaji wa Pato la Taifa (GDP) sekta hiyo imekuwa ikiendelea kudhihirisha ukuaji baada ya kuchangia kaisi cha shilingi 1.3 trillioni ambayo nis awa asilimia 10.1 kwenye mwisho wa mwaka wa serikali Juni 2026.

Kwa upande wake , Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye amesema  katika maadhimisho hayo ya 11 ya wiki ya utafiti na ubunifu ni muhimu nchini kuendelea kuwekeza kwenye tafiti ili kutatua changamoto za kitaifa kwa ustawi wa taifa na watu wake.

“Natoa wito kwa Waziri na serikali kwa ujumla kuendelea kuwatumia wanataaluma wa chuo hiki ni wamesoma kwa kodi za watanzania ni muhimu kuwatumia kwa maendeleo ya nchini na watu wake,” ameongeza Profesa Anangisye.

Amesema chuo hicho ina nafasi katika kuendelea kuzalisha maarifa , kukuza ujuzi ili kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto za kitaifa kwenye sekta ya madini na zingine mtambuka.

Amefafanua kuwa chuo hicho kitaendelea kushirikiana na serikali , sekta binafsi , taasisi za umma , mashirika ya kimataifa na wadau wengine katika uchangiaji wa maarifa , tafiti na ujuzi kwenye sekta mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments