ASKOFU MAKALA AHUBIRI AMANI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


Askofu mstaafu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Daktari Emmanuel Joseph Makala amewaasa wananchi kutunza amani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika siku ya Jumatano ya tarehe 27.11.2024.

Akofu Makala ameyasema hayo leo 24.11.2024 katika ibada ya ubarikio wa wanafunzi wa kipaimara usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga.

"Nawatakieni wiki nzuri kabisa ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa, dumisheni amani. Sio amani tu, Kwa sababu amani ni tunda la haki, dumisheni haki izae amani. Naombeni sana, Kwa sababu kwenye uchaguzi huu kuna uchawi, kuna pesa na kuna shetani."

"Chagueni Mungu, na kwa yeyote yule anayetaka kutuongoza mnatakiwa kutumia nafasi hii kishiriki kikamilifu Kwa sababu ni vibaya sana kuongozwa na mtu ambaye kwanza haukumchagua na haumtaki. Basi tumieni nafasi hii vizuri kabisa na kwa amani."

Ibada hiyo pia imeambatana na tendo kuwaingiza kazini wazee wa kanisa, viongozi wa jumuiya pamoja na wajumbe wa kamati mbalimbali za usharika.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.