YANGA YABADILISHIWA UWANJA NIGERIA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
IKIJIANDAA na mchezo dhidi ya Yanga, Rivers United kutoka Nigeria, imeiandikia barua Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ikiomba ibadilishiwe uwanja.
Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa nchini Nigeria ambapo Rivers United watakuwa wenyeji wa Yanga, Aprili 23, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Rivers United, tayari klabu hiyo imesilisha barua CAF ikiomba kubadilishiwa uwanja.
Mtandano huo ulisema kuwa, katika barua hiyo, wameomba watumie Uwanja wa Adekiye Amiesimaka uliopo katika Mji wa Port Harcourt huko Nigeria.
Taarifa hiyo ilisema kwamba, uwanja huo uliofungiwa awali kwa ajili ya ukarabati, hivi sasa upo tayari kwa ajili ya matumizi.
“Awali tulikuwa tukitumia Uwanja wa Gods Will Akpabio, lakini hivi sasa tumewaomba CAF turudi kwenye Uwanja wa Adekiye Amiesimaka uliopo katika Mji wa Port Harcourt hapa Nigeria.
“Tunaamini kuwa maombi yetu yatakubaliwa na CAF kuutumia uwanja huo tuliouomba,” ilisema taarifa hiyo.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: