MAHAKAMA YATOA MAAMUZI MDOGO KESI YA WABUNGE 19 WA CHADEMA

Halima Mdee na wenzake 18 wafukuzwa rasmi Chadema Mahakama Kuu imeridhia mawakili wa wabunge 19 wakiongozwa na Halima Mdee kuwasilisha mapingamizi yao ya awali ili yasikilizwe kabla ya kuendelea na kesi ya msingi.

Uamuzi huo imetolewa leo Septemba 2, 2022 na Jaji Cyprian Mkeha wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mapingamizi yaliyowasilishwa na wapeleka maombi

Jaji Mkeha baada ya kutoa uamuzi huyo, mjibu maombi wa kwanza, Wakili Pater Kibataka aliiomba mahakama hiyo iwape dakika 15 ili aweze kujadiliana na wenzake.

Jaji Mkeha alikubaliana na ombi la Kibatala na kauhirisha kesi hiyo kwa muda.

Kabla ya kuahirisha shauri hilo kwa muda, Jaji Mkeha alimtaka Kibatala ashauriane na mjibu maombi namba mbili ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Time ya Tafa ya Uchaguzi, kama watakubaliana kuendelea na kesi hiyo kwa muda huu au watakubaliana kuiahirisha.

Idadi ni kubwa ya wafuasi wa pande zote mbili, waliojitokeza katika Mahakama kusikiliza uamuzi huo.

Post a Comment

0 Comments