MWANDISHI WA HABARI WA ITV MKOA WA SHINYANGA APATA AJALI YA GARI

Mwandishi wa habari wa ITV Mkoa wa Shinyanga Frank Mshana amepata ajali jioni hii katika barabara ya Kishapu baada ya gari alilokuwa anasafiria kutoka Shinyanga Mjini kuelekea Kishapu kupasuka tairi na kugonga gema kisha kutumbukia kwenye korongo.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Mshana amesema alikuwa anaelekea Kishapu kutekeleza majukumu yake ya uandishi wa habari.

"Wakati naendelea na safari yangu tairi ya gari ilipasuka, mbele kulikuwa na gari inakuja kwa mwendo kasi, kutokana na tairi kupasuka gari likayumba nikagonga gema kisha gari kutumbukia kwenye korongo. Namshukuru Mungu nimetoka salama japo nasikia maumivu mgongoni, gari imeharibika",amesema Mshana

Post a Comment

0 Comments