
Katika hali isiyo ya kawaida jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Saidi Saidi mkazi wa Morogoro  amejitwalia umaarufu mkubwa baada ya kula kilo mbili za wali na kunywa lita moja ya maji.
Umaarufu huo umekuja kwenye mashindano ambayo hufanyika kila mwaka mjini Morogoro mashindano yajulikanayo kama WALI TONGE NYAMA.
Akihojiwa na mwandishi wetu Saidi alisema hata hivo hakujua kama mashindano hayo yalikuwa siku hiyo kwani asubuhi alikuwa tayari ameshakula maandazi mia na jagi moja la chai.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 Comments