MWANAUME MMOJA AJIKATA UUME WAKE KWA SABABU ZA KIJINGA
Mkazi wa Kijiji cha Itolwa wilayani Chemba Mkoani Dodoma, Juma Juma (34) amelazwa katika kituo cha Afya cha Hamai wilayani Chemba akiwa hoi baada ya kujikata uume wake.
Inadaiwa kuwa Juma amefikia uamuzi huo baada ya kupata ajali na kuteguke kiuno na kusababisha asiwe rijali.
Akizungumzia tukio hilo leo Jumapili Novemba 19, 2021 mjomba wa Juma, Yasini Nkusa amesema tukio hilo la Juma kujikata uume lilitokea Ijumaa nyumbani kwake Kijiji cha Itolwa ambapo alitumia wembe kukata uume wake.
Hali ya majeruhi huyo imeelezwa kuwa mbaya pamoja na kwamba jitihada za madaktari wa Kituo cha Afya Hamai kuendelea kuokoa maisha yake.
Juma ambaye ana mke na watoto watatu alipata ajali ya gari wiki mbili zilizopita.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Itolwa, Daudi Ally amethibitisha tukio hilo akisema mhusika amechukua maamuzi magumu huku akidai kuwa ni tukio la kwanza kutokea Kijijini hapo.
Ametoa wito kwa wananchi kuacha kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuathiri maisha yao.
Mkazi wa kijiji hicho, Maulidi Kijongo amesema ameshangazwa na uamuzi huo akidai hakupaswa kufanya hivyo.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: