MBWANA SAMATTA ACHEKA NA NYAVU TIMU YAKE IKIFUNGWA

KLABU ya Royal Antwerp anayoichezea Mtanzania, Mbwana Samatta imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka Olympiacos katika mchezo wa michuano ya Europa.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Karaiskakis ulikuwa na ushindani na kuifanya timu ya Samatta kushindwa kusepa na pointi hata moja baada ya dakika 90.

Ni mabao ya Youssefi El-Arabi dk ya 52 na Oleg Reabciuck dakika ya 87 alipachika msumari wa maumivu ulioweza kufuta furaha ya kupata pointi moja kwa kuwa Samatta alipachika bao dakika ya 74.

Pia walimaliza dakika 90 akina Samatta wakiwa pungufu baada ya nyota wao Jelle Bataille kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90.

Katika msimamo timu ya Samatta iliyo kundi D inashikilia nafasi ya nne ikiwa haina hata pointi huku nafasi ya kwanza ikiwa mikononi mwa Olympiacos.

Pia ni mashuti 17 yalipigwa na timu ya Samatta huku 16 hayakulenga lango na ni moja tu la Samatta liliweza kulenga lango na ikiwa waya.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.