HII KALI YA MWAKA!! ATEMBEA MTAANI NA BANGO AKITAFUTA MUME WA KUMUOA JIJINI DAR ES SALAAM! WATU WASHANGAA

Picha ya Baby Nai akiwa na bango lake la kutafuta mume mtaani


Mrembo Baby Nai kutoka Buza Temeke amesema anatufuta mume wa maisha wa kumuoa mwenye miaka 20 hadi 70 na kigezo chake anataka awe mstaarabu na mcha Mungu.

Baby Nai ameongeza kusema hii ni siku ya tano kutembea na bango la kutafuta mume mtaani pia haoni shida ya kutembea na bango hilo kwa sababu havunji sheria za nchi.

Mwisho amemaliza kusema akikosa mume anayemtaka Dar es Salaam ataenda Arusha, Mwanza na Mbeya na akikosa hapo ataenda nchini Kenya na Uganda.

Chanzo - EATV

Post a Comment

0 Comments