Wakati dirisha la usajili likikaribia kufunguliwa, tayari vuguvugu lake limeanza kushika kasi kwa timu kuanza kupigana vikumbo kuwania wachezaji watakaozitumikia msimu ujao.
Yanga mabingwa msimu uliopita, wamepania kwelikweli kutengeneza kikosi cha 'maangamizi' hasa baada ya kushindwa kufikia matarajio yake msimu huu.
Tayari Yanga inawajaribu wachezaji wanne wa Kimataifa ili kujiridhisha na uwezo wao kabla ya kuwapa mikataba.
Lakini kubwa ni kwamba kuna taarifa Kocha Mwinyi Zahera huenda akafanikisha usajili wa mlinda lango wa TP Mazembe Vumi Ley Matampi aliye pia kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo.
Mkataba wa mlinda lango huyo na Mazembe inaelezwa kuwa umemalizika na pande mbili zimeshindwa kufikia makubaliano.
Swali la msingi je Yanga bado inahitaji huduma ya mlinda lango wa Kimataifa baada ya kuwa na msimu mmoja na Youthe Rostand?
Naamini kama Vumi Ley Matampi atasajiliwa ni dhahiri itabidi imuache Rostand baada ya msimu mmoja tu.
Lakini wakati huo huo Yanga inae kipa mwenye uwezo wa hali ya juu Benno Kakolanya ambaye mkataba wake unamalizika ndani ya wiki mbili zijazo.
Kama kuna ulazima wa kubadili mlinda lango kwa nini Yanga isimpe Kakolanya mkataba mpya aweze kusaidiana na 'dogo' Ramadhani Kabwili halafu akasajiliwa mlinda lango mwingine wa ndani wa kuongeza ushindani?
Gharama za kumsajili kipa wa Kimataifa ni dhahiri zitakuwa juu ukilinganisha na kipa wa ndani.
Nakumbuka msimu uliopita Simba iliamua kuachana na mlinda lango Mghana, Daniel Agyei licha ya ubora wake na kumsajili Aishi Manula huku nafasi yake wakiongeza mchezaji mwingine wa Kimataifa
0 Comments